Back

ⓘ Historia ya Kuba. Kuba ilikuwa koloni la Hispania kuanzia kufika kwa Kristoforo Kolumbus mwaka 1492 hadi mwaka 1898. Wenyeji asilia walikuwa Waindio lakini weng ..                                     

ⓘ Historia ya Kuba

Kuba ilikuwa koloni la Hispania kuanzia kufika kwa Kristoforo Kolumbus mwaka 1492 hadi mwaka 1898. Wenyeji asilia walikuwa Waindio lakini wengi wao walikufa haraka kutokana na magonjwa kutoka Ulaya na ukali wa ukoloni wa Wahispania.

Baadaye uchumi wa mashamba makubwa ya sukari ulijengwa kwa nguvu ya watumwa kutoka Afrika.

Kuanzia miaka ya 1860 watu wa Kuba walianza kupinga utawala wa Hispania na pia kudai mwisho wa utumwa. Mnamo 1898 manowari ya Kimarekani SS Maine ililipuka katika bandari ya Havana na tukio hili lilikuwa msingi kwa Marekani kutangaza hali ya vita dhidi ya Hispania. Marekani ilishinda katika Vita vya Marekani dhidi ya Hispania na kutawala kisiwa katika miaka iliyofuata.

                                     

1. Uhuru chini ya usimamizi wa Marekani

Baada ya majadiliano marefu Kuba ilipata uhuru wake kuanzia mwaka 1902 lakini ilipaswa kukubali mkataba uliotunza haki ya Marekani kungilia kati mambo ya ndani na kuipa Marekani eneo kwa kituo cha kijeshi.

Hadi mwaka 1934 Marekani iliingilia mara mbili na kupindua marais wawili wa Kuba, ama kwa kutuma jeshi lake au kwa kutumia wanajeshi wa Kuba. Eneo la Guantanamo Bay kusini mwa Kuba limebaki hadi leo kama kituo cha kijeshi cha Marekani.

Mkataba mpya kati ya Marekani na Kuba wa mwaka 1934 uliongeza haki za Kuba. Wakati huohuo uasi wa kijeshi ulimwingiza sajenti Fulgencio Batista kwenye uwanja wa siasa. Batista alijipandisha cheo hadi kanali akashika mamlaka yote ya kijeshi na kuteua marais waliotekeleza matakwa yake.

Mwaka 1940 alichaguliwa mwenyewe kuwa rais, akarudi 1952 kwa kugombea tena urais lakini, baada ya kuona angeshindwa, alipindua serikali kwa njia ya uasi wa kijeshi akasimamisha katiba na kuwa dikteta wa Kuba hadi mwaka 1959. Chini ya serikali ya Batista ulaji rushwa na athira ya kiuchumi ya makampuni ya Kimarekani viliongezwa. Ukali wa utawala na mauaji ya wapinzani wengi vilisababisha kutokea kwa vikundi vilivyokuwa tayari kupinga serikali ya dikteta kwa silaha.

                                     

2. Mapinduzi ya 1959

Tangu mwaka 1953 mwanasheria Fidel Castro alijaribu kukusanya wafuasi kwa mapinduzi akishambulia kituo cha kijeshi cha Moncada akakamatwa na kutupwa jela.

Mwaka 1955 wafungwa walisamehewa na Batista. Castro alianza tena kukusanya wafuasi waliobaki katika "Harakati ya 26 Julai" MR-26-7. Maandamano ya upinzani yalifuatwa na polisi kukamata wanaharakati. Fidel Castor pamoja na nduguye Raul walikimbia Meksiko. Hapo alikutana na tabibu Mwargentina Che Guevara.

Mwaka 1956 Castro pamoja na Guevara na wafuasi 80 walivuka bahari kwa jahazi "Granma" wakajificha katika milima ya Sierra Madre. Kutoka huko walianza kushambulia vikosi vya jeshi la Batista.

Polepole idadi ya wapiganaji waliojiunga nao iliongezeka na wanajeshi wa serikali mara nyingi walihamia upande wa Castro. Tarehe 1 Januari 1959 dikteta Batista alikimbia na kuondoka Kuba, vikosi wa wanamapinduzi waliingia Havana.

                                     

3. Baada ya mapinduzi

Mwanzoni Castro alionekana kama msemaji mkuu wa mapinduzi akimtangaza mwanasheria Manuel Urrutia kama rais mpya. Fidel alichukua cheo cha waziri mkuu katika Februari 1959.

Hapo mwanzoni serikali mpya ilikuwa muungano wa wapinzani wa udikteta na wanamgambo kutoka milimani. Uchaguzi wa vyama vingi ulitangazwa kama shabaha mojawapo ya kurudisha demokrasia. Katika miezi iliyofuata wanasiasa wenye mwelekeo wa kati waliondolewa polepole na Castro aliongeza idadi ya Wamarxisti katika vyeo vya juu.

Kuanzia 1960 na baada ya jaribio la Marekani kumpindua Castro huyu aliongeza mwelekeo wake wa kisoshalisti. Baada ya kupingwa na Marekani, Castro alitafuta ushirikiano na usaidizi kutoka Urusi wa kikomunisti.

Castro alitangaza siasa ya kikomunisti akaendelea kutawala bila uchaguzi huru hadi alipojiuzulu mnamo Februari 2008 kwa sababu za afya. Baada yake aliongoza mdogo wake, Raul Castro, hadi mwaka 2018 Miguel Díaz-Canel alipochaguliwa kuwa rais wa nchi.                                     
 • Kwa kuba pia: kubba kama sehemu ya jengo tazama Kuba jengo - Kuba pia: Kyuba kwa Kihispania: Cuba ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi
 • Kuba Kar. قبة kubba ni sehemu ya jengo inayoonekana kama nusu tufe iliyoko juu ya jengo fulani. Ni sifa inayolenga kuonyesha umuhimu maalum wa jengo
 • dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko. Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania. Baada ya mlipuko
 • pia kuboma kuba juu ya kaburi la Mtume Muhamad lakini walishindwa, wakaendelea kubomoa makaburi yaliyopambwa ya wenzake Muhamad. Idadi ya Wahiji ilipungua
 • mji mkuu na mji mubwa wa Kuba kwenye 23 8 N 82 23 W. Kuna wakazi milioni 2.2. Tangu 1982 mji wa kale umepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Mji kwa
 • Guantanamo Bay au Hori ya Guantanamo kwa Kihispania Bahía de Guantánamo ni hori ya Bahari ya Karibi inayoingia kusini mwa kisiwa cha Kuba yenye upana wa km
 • makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino. Vita hii ilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali.
 • serikali ya Afrika Kusini ikaanza kuchukua hatua za kuandaa uhuru wa eneo hili, lakini vita kati ya jeshi lake, SWAPO na wanajeshi wa Angola na Kuba iliendelea
 • cha Antili Kubwa baada ya Kuba na iko upande wa magharibi wa Puerto Rico, karibu na Kuba na Jamaica. Wenyeji kwa ajili ya kisiwa chao hutumia pia jina
 • Zaire Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba na Nicaragua. Tarehe 22 Machi
 • mashariki ya nchi. Umbo lake ni rasi inayoanza Marekani bara kuelekea Kuba Upande wa magharibi ni maji ya ghuba ya Meksiko na upande wa mashariki maji ya Atlantiki
                                     
 • kufa kwa sababu ya kansa iliyosababishwa na mnururisho. Mji ukajengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Jengo la Kuba ya Bomu ya nyuklia ni ghofu
 • vingine nje ya Trinidad vilianza kufikiwa na watu kuanzia miaka ya 3000 KK na akiolojia imegundua mabaki ya kipindi hicho huko Barbados, Kuba Curaçao na
 • mwaka 1868 BK Baada ya Kristo 11 Juni - Tekle Giyorgis II alitangazwa kuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi. 10 Oktoba - Nchi ya Kuba inapata uhuru kutoka Hispania
 • funguvisiwa la Karibi na eneo la ng ambo la Uingereza katika Bahari ya Karibi upande wa kusini wa Kuba na upande wa magharibi wa Jamaika. Eneo lake ni visiwa vitatu
 • visiwani katika bahari ya Karibi: Antigua na Barbuda Aruba Bahamas Barbados Dominica Jamhuri ya Dominika Grenada Haiti Jamaika Korsou Kuba Saint Kitts na Nevis
 • na majeshi ya Kuba Ujerumani wa mashariki na Yemeni. Usaidizi mwingi kutoka Nchi za Kikomunisti uliwezesha Ethiopia kudumisha mojawapo ya majeshi kubwa
 • Jardines del Rey ni funguvisiwa la bahari ya Karibi karibu na Kuba
 • Sabana - Camaguey ni funguvisiwa la bahari ya Karibi karibu na Kuba Visiwa vyote ni kama 2, 517 vilivyozagaa katika eneo la kilometa mraba 75, 000.
 • anafika kwenye visiwa vya Karibi akiamini ya kwamba amefika Uhindini. 28 Oktoba - Kristoforo Kolumbus anafika Kuba 25 Julai - Papa Innocent VIII Wikimedia
 • Jardines de la Reina ni funguvisiwa la bahari ya Karibi kusini kwa Kuba
                                     
 • Pico Turquino ni mlima mrefu zaidi nchini Kuba Una kimo cha mita 1, 975 juu ya UB. Orodha ya milima
 • Canarreos ni funguvisiwa la bahari ya Karibi kusini kwa Kuba Visiwa vyote ni kama 350 ambavyo kati yake kikubwa kabisa ni Isla de la Juventud.
 • Isla de la Juventud zamani Isla de Pinos ni kisiwa kikubwa kuliko vyote vya karibu na Kuba Kina eneo la kilometa mraba 2, 419 na wakazi 86, 420.
 • na visiwa vingi vidogo. Kuba Hispaniola yenye nchi mbili za Haiti na Jamhuri ya Dominika Jamaika Puerto Rico Kuba nchi Kuba kisiwa Archipiélago de
 • nchi ya visiwani katika bahari ya Atlantiki, kaskazini kwa Kuba na mashariki kwa Florida Marekani Visiwa hivyo 700 na zaidi viko nje ya Bahari ya Karibi
 • kati ya visiwa vya Kuba na Jamaika mwenye urefu wa 7, 686 m chini ya UB. Kuna hori za bahari na ghuba mbalimbali kama ghuba ya Venezuela na ghuba ya Honduras
 • katika Kuba ulipokea wakimbizi wengi kutoka kisiwa kile na kuwa kitovu cha utamaduni wenye lugha ya Kihispania katika Marekani. Sehemu muhimu ya uchumi
 • nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini kwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili
 • Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1972 3 Juni - Raul Castro, rais wa nchi ya Kuba tangu 2006 15 Agosti - Richard Heck, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia

Users also searched:

historia ya kuba, hispania. historia ya kuba,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →