Back

ⓘ Historia ya Haiti. Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak. Baada ya kufika kwa Kristoforo Kolumbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana n ..                                     

ⓘ Historia ya Haiti

Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak.

Baada ya kufika kwa Kristoforo Kolumbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana na magonjwa ya Ulaya ambayo hawakuzoea na kukosa kinga dhidi yake, lakini pia kutokana na kutendwa kwa unyama na mabwana wapya.

Wahispania walianzisha mashamba kwa kutegemea kazi ya watumwa kutoka Afrika.

Mnamo mwaka 1600 Waindio wachache tu walibaki kutoka malakhi wakati wa Kolumbus wakapotea kabisa kwa njia ya kuoa au kuolewa na Wazungu na Waafrika.

                                     

1. Ukoloni wa Ufaransa

Katika karne ya 17 Wafaransa walifika kisiwani wakanunua theluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujenga uchumi wa mashamba makubwa, hasa ya miwa. Koloni la Saint-Domingue lilikuwa koloni tajiri la Ufaransa katika Amerika.

                                     

2. Mapinduzi ya Ufaransa

Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789 koloni lilikuwa na wakazi wa aina nne:

 • Wazungu, hasa Wafaransa, waliokuwa mabwana lakini walikuwa na tofauti kubwa kati yao: wengine tajiri sana wengine maskini - jumla takriban watu 32.000
 • Wamaroni walikuwa watumwa wakimbizi walioishi mlimani katika pori - idadi yao haijulikani lakini hawakuwa wengi.
 • machotara na Weusi huru ambao walikuwa raia wa daraja ya pili; wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa - jumla watu 28.000
 • watumwa wenye asili ya Kiafrika - jumla watu 500.000

Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwa haki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya machotara wenye mali ya kukubaliwa kama raia kamili wenye haki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.

                                     

3. Mapinduzi ya Haiti

Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada wa Uingereza na Hispania wakichukia mapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na Weusi huru wenye elimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hao bila sheria za Ufaransa utakuwa mbaya kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza mapinduzi.

Kiongozi wao alikuwa Toussaint LOuverture aliyefaulu kushika serikali ya koloni tangu mwaka 1798. Awali alipigania jeshi la Ufaransa; baada ya bunge la Paris kutangaza mwisho wa utumwa alishirikiana na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye mashamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.

Toussaint LOuverture alishinda pia Waingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa wa Paris na mwaka 1801 akateka kaskazini mwa kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawala Hispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.

Lakini mnamo mwaka 1802 siasa ya Paris ilibadilika na mtawala Napoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola katika hali ya awali akatuma jeshi kubwa la askari 40.000. LOuverture alikamatwa alipokubali kushauriana na jenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakini makamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia kuhusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianza vita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Dessalines alitangaza uhuru wa koloni tarehe 1 Januari 1804 kwa jina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi".                                     
 • Haiti ni nchi kwenye kisiwa cha Karibi cha Hispaniola. Eneo la Haiti ni takriban theluthi moja ya Hispaniola yote. Sehemu kubwa ya kisiwa inaunda nchi
 • Play media Kreyol Ayisien au Krioli ya Haiti ni lugha ya Krioli iliyozaliwa nchini Haiti na kuwa moja ya lugha rasmi katika nchi hiyo. Ndiyo Krioli kubwa
 • ilivyokuwa upande wa Haiti chini ya utawala wa Ufaransa. Damu ya Kizungu imechangia zaidi, wakati ile ya Kiindio imechangia kidogo kuliko ya Kiafrika. Santo
 • Jamhuri ya Dominikana ni nchi iliyoko kwenye kisiwa cha Bahari ya Karibi cha Hispaniola na inayopakana na Haiti tu. Hispaniola ni kisiwa kikubwa cha pili
 • Navassa ni kisiwa cha bahari ya Karibi karibu na Haiti ambacho kinadaiwa na nchi hiyo tangu mwaka 1801 kuwa ni chake lakini kinatawaliwa na Marekani tangu
 • Port - au - Prince ni mji mkuu wa Haiti mwenye wakazi milioni 2. Iko upande wa magharibi wa kisiwa cha Hispaniola katika hori ya Gonave. Mji ulianzishwa na Wafaransa
 • Hispaniola Haiti na Jamhuri ya Dominika Île de la Tortue Haiti Île de la Gonâve Haiti Île Grande Cayemite Haiti Île à Vache Haiti Cayos Siete
 • inahusu mwaka 1804 BK Baada ya Kristo 1 Januari - Haiti inatangaza uhuru wake kutoka Ufaransa kama Jamhuri ya watu weusi ya kwanza na taifa huru la pili
 • Idadi ya lugha za aina hiyo ni walau 100, na nyingi kati yake zimetokana na lugha za Ulaya. Krioli kubwa zaidi ni ile ya Haiti yenye wasemaji zaidi ya milioni
 • za visiwani katika bahari ya Karibi: Antigua na Barbuda Aruba Bahamas Barbados Dominica Jamhuri ya Dominika Grenada Haiti Jamaika Korsou Kuba Saint Kitts
                                     
 • Lilavach ni kisiwa cha bahari ya Karibi karibu na Haiti Kisiwa kina eneo la kilometa mraba 52 na wakazi 15, 000.
 • Latoti ni kisiwa cha bahari ya Karibi karibu na Haiti Kisiwa kina eneo la kilometa mraba 180 na wakazi 25, 936.
 • Gonave ni kisiwa cha bahari ya Karibi karibu na Haiti Kisiwa kina eneo la kilometa mraba 690 na wakazi 87, 077.
 • Kayimit ni visiwa pacha vya bahari ya Karibi karibu na Haiti Kisiwa kina eneo la kilometa mraba 45 na wakazi 18, 000.
 • ng ambo wa Ufaransa Hispaniola chenye nchi za Jamhuri ya Dominika na Haiti Jamaika Korsou sehemu ya Ufalme wa Nchi za Chini Kuba Martinique mkoa wa ng ambo
 • Amerika, na cha kumi duniani. Kisiwani kuna nchi huru mbili: Haiti upande wa magharibi na Jamhuri ya Dominikana upande wa mashariki. Wikimedia Commons ina media
 • Kutokana na historia hii visiwa vingi vina idadi kubwa ya watu wenye asili ya kiafrika kama kwa mfano kisiwa cha Hispaniola chenye nchi mbili za Haiti na Jamhuri
 • nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini kwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili
 • ya mafanikio ya uasi wa watumwa katika historia Theluthi mbili zilizobaki za Hispaniola zilishindwa na vikosi vya Haiti mnamo 1821 na kuwa chini ya Haiti
                                     
 • katika mazingira ya Haiti kanisa kuu la Port - au - Prince, Haiti Touchdown Jesus karibu na Hesburgh Library. Mchoro wa Pietro Perugino, aina ya Stabat Mater
 • Kati ya Krioli hizo, ile ya Haiti na ile ya Shelisheli ni lugha rasmi nchini. Kilatini kilikuwa lugha rasmi ya utawala, elimu na biashara ya Dola la
 • Yanaon Lugha ya kitaifa na lugha rasmi katika maeneo ya kifaransa ya Polynesia ya Kifaransa na Kaledonia Mpya Lugha rasmi ya Haiti Lugha ya utawala katika
 • Wayback Machine. for We Are the World 25 for Haiti Official music video of We Are the World 25 for Haiti at Youtube.com Kigezo: Harry Belafonte Kigezo: Stevie
 • lugha ya taino kwenye kisiwa cha Haiti Ilhali historia ya kufika kwa muhindi katika Afrika ya Mashariki haijulikani kikamilifu kuna pia uwezekano ya kwamba
 • huhesabiwa katika Amerika ya Kati kwa sababu za kiutamaduni Antigua na Barbuda Bahamas Barbados Dominica Jamhuri ya Dominika Grenada Haiti Jamaika Kuba Saint
 • Mahema ya wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Haiti mwaka 2010 Hema la wafugaji Waarabu huko Syria Hema kubwa la sarakasi Barum, Ujerumani Mahema ya kijeshi
 • yalikuwa Ubelgiji, Bolivia, Brazil, China, Kuba, Ekuador, Ugiriki, Guatemala, Haiti Ufalme wa Hijaz Uarabuni Honduras, Liberia, Nikaragua, Panama, Peru
 • Wadogo 6 wa kwanza walifika Amerika kisiwa cha Hispaniola, leo Dominikana Haiti mwaka 1493 na kuanza kuwahubiria wazalendo. Wengine wakafuata mapema na
 • 1798 Nusu ya magharibi ya Hispaniola ilikuwa koloni ya Haiti ya Ufaransa mwaka 1697. Tangu uhuru wa koloni za Uingereza katika Amerika ya kaskazini zilizounda


                                     
 • ulioitwa sasa Jamhuri ya Biafra Nchi chache tu zilitambua nchi mpya zilikuwa Gabon, Haiti Côte d Ivoire, Tanzania na Zambia. Vita ya miaka mitatu ilianza

Users also searched:

historia ya haiti, hispania. historia ya haiti,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →