Back

ⓘ Ole Romer. Ole Christensen Romer alikuwa mtaalamu wa astronomia kutoka nchini Denmark ambaye mnamo 1676 alifanya vipimo vya kwanza vya Kasi ya nuru. Romer pia a ..Ole Romer
                                     

ⓘ Ole Romer

Ole Christensen Romer alikuwa mtaalamu wa astronomia kutoka nchini Denmark ambaye mnamo 1676 alifanya vipimo vya kwanza vya Kasi ya nuru.

Romer pia alibuni kipimajoto cha kisasa kinachoonyesha halijoto kati ya nukta mbili ambazo ni sehemu ambapo maji huchemka na kuganda.

Katika vitabu vya sayansi, tahajia mbadala kama "Roemer", "Römer", au "Romer" ni kawaida.

                                     

1. Maisha

Romer alizaliwa mnamo 25 Septemba 1644 mjini Aarhus. Wazazi wake walikuwa mfanyabiashara na nahodha Christen Pedersen aliyefariki 1663, na Anna Olufsdatter Storm 1610 hivi - 1690, binti wa mjumbe wa halmashauri ya mji. Tangu mwaka 1642, Christen Pedersen alikuwa akitumia jina la Romer, ambalo linamaanisha kwamba alitokea kisiwa cha Denmark cha Romo, ili kujitofautisha na watu wengine kadhaa walioitwa pia Christen Pedersen.

Kuna habari chache kuhusu Ole Romer kabla ya 1662, alipohitimu kutoka kwa shule ya kanisa kuu la Aarhus. Kutoka hapo alihamia Kopenhagen akasoma hisabati na astronomia kwenye Chuo Kikuu cha Kopenhagen. Mlezi wake kwenye Chuo Kikuu alikuwa profesa Rasmus Bartholin alieyechapisha ugunduzi wake wa upindaji maradufu ya mwanga katika fuwele mnamo 1668, wakati Romer alikuwa akiishi nyumbani kwake. Romer alipewa fursa ya kujifunza hisabati na astronomia akitumia maandiko ya Tycho Brahe, kwani Bartholin alikuwa amepewa jukumu la kuyaandaa kwa uchapishaji.

Baada ya kuhitimu chuo Romer aliajiriwa na serikali ya Ufaransa: mfalme Louis XIV alimfanya mwalimu wa mwanawe alishiriki pia katika ujenzi wa chemchemi za mapambo nzuri kwenye jumba la Versailles.

Mnamo 1681 Romer alirudi Denmark akateuliwa kuwa profesa wa astronomia katika Chuo Kikuu cha Kopenhagen.

Romer alipewa pia nafasi ya mwanahisabati mkuu wa kifalme na hapo alianzisha mfumo wa kwanza wa kitaifa wa vipimo sanifu katika Denmark mnamo 1 Mei 1683. Pamoja na vipimo vingine alifafanua maili mpya ya Kidenmark kuwa na futi 24.000 karibu mita 7.532.

Mnamo mwaka 1700 Romer alimshawishi mfalme kukubali kalenda ya Gregori kwa matumizi katika ufalme wa Denmark-Norwei. Hili ni jambo ambalo Tycho Brahe alishindwa kuanzisha miaka mia moja kabla yake.

Romer alibuni moja ya skeli za kupima halijoto za kwanza. Daniel Gabriel Fahrenheit alimtembelea mnamo 1708 na kuendeleza skeli ya Romer, na matokeo yake yalikuwa skeli ya joto ya Fahrenheit inayotumika hadi leo katika nchi kadhaa ingawa mahali pengi skeli ya selsiasi imechukua kipaumbele.

Romer pia alianzisha vyuo kwa mabaharia katika miji kadhaa ya Denmark.

Mnamo mwaka wa 1705, Romer alipewa pia kazi ya kusimamia polisi ya Kopenhagen, nafasi ambayo aliishikilia hadi kifo chake mnamo 1710. Kama moja ya maazimio yake ya kwanza, alifukuza watumishi wote wote, akiamini kuwa ari yao ilikuwa duni mno. Alibuni taa za kwanza za barabarani taa za mafuta mjini Kopenhagen. Alijitahidi kudhibiti waombaomba, watu wasio na kazi, na makahaba wa Kopenhagen.

Romer alitunga sheria za ujenzi wa nyumba mpya, akatengeneza mfumo wa maji na maji taka ya mji, akapatia walinzi moto vifaa vipya akashawishi serikali ya mji kupanga mitaa imara iliyofunikwa kwa mawe ya vibbamba.

Romer alifaRIKI akiwa na umri wa miaka 65 mnamo 1710. Alizikwa katika Kanisa Kuu la Kopenhagen.

                                     

2. Romer na kasi ya nuru

Hadi siku za Romer wataalamu wengi waliona nuru haina kasi, wakiamini inafika mara moja kwa mtazamaji. Lakini wengine walihisi inaweza kuwa na mwendo.

Mnamo 1671 Romer akajiunga na Jean Picard kutazama kupatwa kwa Io, mwezi wa Mshtarii, kwa kipindi cha miezi kadhaa, wakati Giovanni Domenico Cassini alitazama matukio ya kupatwa yaleyale huko Paris, Ufaransa. Io inazunguka Mshtarii kila baada masaa 42½ kwa hiyo kwa mtazamaji wa duniani inafunikwa na sayari hiyo kwa sehemu ya obiti yake, yaani inapatwa na Mshtarii.

1668 Cassini aliwahi kutoa jedwali inayotabiri ufuatano na wakati wa kuona kupatwa kwa Io. Lakini wakati wa kutazama Io na Mshtarii kuna tofauti ya dakika kadhaa kati ya jedwali yake na kupatwa jinsi kunavyotazamwa.

Romer alitambua kwamba mabadiliko haya yako tofauti kulingana na majira ya mwaka. Romer aliamini kwamba kasi ya obiti ya Io haibadiliki; ilhali alijua umbali kati ya Mshtarii na Dunia inayobadilika kidogo kulingana na mwendo wao zikizunguka Jua, alitambua kwamba wakati Dunia na Mshtarii zinaongeza umbali kati yake, muda wa kupatwa ulikuwa mkubwa kidogo. Kinyuma chake wakati Dunia na Mshtarii zinasogea karibu zaidi, muda wa kupatwa wa Io ulipungua kidogo.

Romer aliwaza kwamba vipimo hivi vinaweza kuelezwa kama nuru ina kasi maalumu aliyoendelea kukadiria. Aliona nuru ilitembea kati ya dakika 10 hadi 11 kutoka Io hadi duniani, kutegemeana na umbali.

Wakati wa maisha yake, wataalamu bado walivutana kati yao kama nuru kweli ina kasi. Lakini hasa pale Uingereza wanaastronomia kama Christiaan Huygens na Isaac Newton walivutwa na makadirio ya Romer na kwa kutumia hesabu zake waliweza tayari kupiga hesabu kuwa nuru ya Jua inahitaju takriban dakika nane kufika duniani, na kipimo hiki kilifanana tayari na elimu yetu ya leo.

                                     

3. Vyanzo

  • MacKay, R. Jock; Oldford, R. Wayne 2000. "Scientific Method, Statistical Method and the Speed of Light". Statistical Science 15 3: 254–278.
. Mostly about A.A. Michelson, but considers forerunners including Romer.
  • Axel V. Nielsen 1944. Ole Romer, en Skildring af hans Liv og Gerning in da. Nordisk Forlag.
                                     

4. Viungo vya nje

  • Jumba la kumbukumbu la Kroppedal
  • Romer na Kanuni ya Doppler. maelezo zaidi juu ya matokeo ya Romer
  • media kuhusu Ole Romer pa Wikimedia Commons
  • Kidenmark Fysikeren Ole Romer kwa Kidenmaki
  • Démonstration touchant le mouvement de la lumière
  • Roemer, Ole Christensen katika Galileo Project
  • Ole Romer kwenye noti 50 ya pesa ya Kroner

Users also searched:

ole romer, kanuni. ole romer, ole rømer,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →