Back

ⓘ Bakteriolojia. Bakteria waligunduliwa mara ya kwanza na Antonie van Leeuwenhoek mwaka 1676, kwa kutumia hadubini ya lensi moja ya muundo wake mwenyewe. Aliwaita ..Bakteriolojia
                                     

ⓘ Bakteriolojia

Bakteria waligunduliwa mara ya kwanza na Antonie van Leeuwenhoek mwaka 1676, kwa kutumia hadubini ya lensi moja ya muundo wake mwenyewe. Aliwaita "animalcules" na alichapisha habari za utafiti wake kwenye msururu wa barua kwa Shirika la Muungano wa Mfalme.

Jina bacteriam lililetwa miaka mingi baadaye, na Christian Gottfried Ehrenberg katika mwaka 1838.

Mwaka 1859 Louis Pasteur alionyesha kuwa mchakato wa kuchachusha unasababishwa na ukuaji wa vijiumbe, na kwamba ukuaji huo si wa kizazi cha kujianzia. Pamoja na mwenzake, Robert Koch, Pasteur alikuwa wa kwanza kuitetea nadharia ya kijidudu kisababishi cha ugonjwa.

Robert Koch alikuwa mwanzilishi wa taaluma ya uuguzi wa mikrobiolojia na alishughulikia kipindupindu, kimeta na kifua kikuu. Katika utafiti wake wa kifua kikuu, Koch hatimaye alithibitisha nadharia ya kijidudu, ambayo ilimfanya atunukiwe Tuzo la Nobel mwaka 1905. Katika madai yake, Koch aliweka vigezo vya kutathmini kama kiumbehai ndiye husababisha ugonjwa, na madai hayo yanatumika mpaka leo hii.

Ingawa katika karne ya 19 ilijulikana kwamba bakteria ndio chanzo cha magonjwa mengi, hakuna matibabu yoyote ya viuabakteria yaliyopatikana. Katika mwaka 1910, Paul Ehrlich alitengeneza kiuavijasumu cha kwanza, kwa kubadilisha rangi ambazo kwa kuchagua zilitia mawaa Treponema pallidum, spirokaeti ambayo husababisha kaswende katika mchanganyiko ambao uliua kisababishi magonjwa. Ehrlich alikuwa ametuzwa Tuzo la Nobel mwaka 1908 kwa kazi yake kuhusu elimu ya kingamaradhi, na alianzisha matumizi ya madoa ili kuchunguza na kubaini bakteria, na kazi yake ilijikita kwenye misingi ya doa la Gram na doa la Ziehl-Neelsen.

Mafanikio makubwa katika utafiti wa bakteria yalikuwa kutambuliwa kwa Carl Woese mwaka 1977 kwamba akea walitokana na mabadiliko tofauti na yale ya bakteria. Uanishaji huo mpya wa jamii ya filojenetikia ulikitwa kwenye misingi ya kufululizwa kwa ribosomu RNA 16S, ukagawa prokaryota katika makundi mawili yenye mageuko tofauti, kama mojawapo ya sehemu ya mifumo ya domeni tatu.

                                     
  • Alitumia miaka sita nchini Ujerumani akisoma chini ya usimamizi wa mwana bakteriolojia Robert Koch. Kwa wakati huo aliweza kutenganisha bakteria anayesababisha
  • utaratibu Taaluma ya Bakteria. Kamati ya Kimataifa juu ya Utaratibu Wa Bakteriolojia ICSB ndiyo hulinda kanuni za kimataifa za kuwapa majina makundi mbalimbali
  • hadubini vidubini na mwingiliano wao na viumbe wengine wanaoishi Bakteriolojia - utafiti wa bakteria Mikolojia - utafiti wa kuvu Virolojia - utafiti
  • Mikrobiolojia ina matawi yake, yakiwemo virolojia, mukolojia, parasitolojia na bakteriolojia Bakteria ziligunduliwa mara ya kwanza na Antonie van Leeuwenhoek mwaka
                                     
  • Kaswende ing. syphilis ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa ambayo inasababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum. Katika hatua za mwanzo

Users also searched:

bakteriolojia, jamii. bakteriolojia,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →