Back

ⓘ Kanisa la Ungamo lilikuwa harakati ndani ya Uprotestanti wa Ujerumani wakati wa utawala wa Adolf Hitler. Ilipinga juhudi zilizofadhiliwa na serikali ya Wanazi z ..Kanisa la Ungamo
                                     

ⓘ Kanisa la Ungamo

Kanisa la Ungamo lilikuwa harakati ndani ya Uprotestanti wa Ujerumani wakati wa utawala wa Adolf Hitler. Ilipinga juhudi zilizofadhiliwa na serikali ya Wanazi za kuunganisha makanisa yote ya Kiprotestanti kuwa kanisa moja la kushikamana na serikali yao.

                                     

1. Mandharinyuma

 • Waprotestanti hao walikuwa wakristo walioandikishwa katika makanisa ya kieneo yaliyowahi kuwa makanisa rasmi ya kidola hadi mwaka 1918. Baada ya mapinduzi ya Ujerumani ya 1918 dola na makanisa yalitengwa. Kidhehebu makanisa hayo yalikuwa ama makanisa ya kilutheri, makanisa ya kireformed au makanisa ya maungano yaliyounganisha sharika za kilutheri na za kireformed.
 • Kanisa kubwa lilikuwa Kanisa la Kiinjili katika Prussia lenye wakristo milioni 18.
 • Idadi ya wachungaji wa Kiprotestanti: 18.000
 • Idadi ya hawa walioshikamana sana na kikundi cha kanisa la "Kukiri Kanisa" kufikia 1935: 3000
 • Idadi ya hawa walioshikamana sana na kikundi cha kanisa la "Kikristo cha Kijerumani" kama cha 1935: 3000
 • Idadi ya hawa waliokamatwa wakati wa 1935: 700
 • Mnamo mwaka 1933 idadi ya wakristo waprotestanti nchini Ujerumani ilikuwa milioni 45 kati ya jumla ya wakazi milioni 78 waliohudumiwa na wachungaji 18.000.
 • Idadi ya hizi ambazo hazijafungamana sana au kushikamana na kikundi chochote: 12.000
 • Jumla ya wakazi wa Ujerumani: 65 milioni
 • Idadi ya Wayahudi nchini Ujerumani: 525.000

Baada ya mapinduzi ya 1918 maelewano yalifikiwa: kusingekuwa tena na makanisa ya kidola, lakini makanisa yalibaki mashirika ya umma yaliendelea kupokea sehemu ya ruzuku kutoka kwa serikali kwa huduma walizofanya kama kuendesha hospitali, chekechea n.k. Kanisa lilipaswa kuachana na usimamizi wa shule. Kwa upande mwingine serikali iliendelea kukusanya michango kutoka wanachama wa kanisa kutoka kwa walipa ushuru walioandikishwa kama washirika wa kanisa na waligawa fedha hizi kwa makanisa. Ada hizi zilikuwa, na hadi leo zinatumika kufadhili shughuli za kanisa. Idara za theolojia katika vyuo vikuu viliendelea kuwapo, na mafundisho ya dini shuleni yaliendelea wakati wazazi waliweza kuondoa watoto wao. Haki zilizokuwa zikishikiliwa na wafalme katika Dola ya Ujerumani zilikabidhiwa kwa mabaraza ya kanisa na sinodi.

Kwa hivyo, katika kipindi hiki cha kwanza cha Jamhuri ya Weimar, mnamo 1922, makanisa ya Kiprotestanti huko Ujerumani yaliunda Shirikisho la Kanisa la Kiinjili la Ujerumani lenye makanisa wanachama 28 ya kieneo. Mfumo huu wa shirikisho uliruhusu uhuru mwingi wa kieneo katika utawala wa Uprotestanti wa Ujerumani. Iliruhusu pia kuanzoishwa kwa sinodi au bunge la kanisa la kitaifa ambalo lilikuwa jukwaa la majadiliano na ambalo lilijaribu kusuluhisha mizozo ya kitheolojia na kiutawala.

                                     

1.1. Mandharinyuma Utawala wa Wanazi

Waprotestanti wengi walipigia kura Wanazi katika uchaguzi 1932 na 1933. Katika maeneo penye Wakatoliki wengi kura ya Wanazi ilikuwa duni kulingana na maeneo ya Waprotestanti. Makanisa ya Kiprotestanti hayakupinga kimsingi itikadi ya Hitler. Waprotestanti wengi walizoea wazo la serikali yenye madaraka mengi na uhusioano wa karibu baina ya serikali na kanisa, jinsi ilivyowahi kuwepo hadi mwaka 1918, miaka michache iliyopita. Waprotestanti wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu jamhuri ya Weimar na demokrasia. Wengi walishikamana na vyama vilivyochora picha nzuri ya miaka iliyopita chini ya wafalme wa Ujerumani.

Idadi ndogo ya viongozi Waprotestanti, kama vile Karl Barth, Dietrich Bonhoeffer na Wilhelm Busch, walipinga Wanazi juu ya kanuni za maadili na kitheolojia; hawangeweza kupatanisha madai ya serikali ya Wanazi kwa udhibiti kamili juu ya jamii upande mmoja na mamlaka kuu inastahili kuwa upande wa Mungu katika imani yao kwa upande mwingine.

                                     

1.2. Mandharinyuma Harakati ya "Wakristo Wajerumani"

Miaka michache kabla ya 1933 ilitokea harakati ya wafuasi wa Hitler kati ya wachungaji na Wakristo wa Kiprotestanti. Walianza kujipanga kama chama ndani ya kanisa na kushiriki katika uchaguzi wa sinodi na mabaraza ya wazee wa sharika wa 1931 katika kanisa la Prussia.

Wakristo Wajerumani walikubali shabaha ya Wanazi ya "kuratibu" makanisa ya Kiprotestanti ya kieneo kuwa kanisa kubwa moja ya kitaifa lililolingana na itikadi ya "Taifa moja, Dola, moja, Kiongozi mmoja" ya Wanazi.

                                     

1.3. Mandharinyuma Kuundwa Kanisa Jipya la Kitaifa Deutsche Evangelische Kirche

Wakati Wanazi walipochukua madaraka kwenye Januari 1933, kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani lilikuwa shirikisho la makanisa huru ya kieneo pamoja na urithi wao wa Kilutheri, kireformed na kimaungano.

Kwenye mwezi wa Aprili 1933 uongozi wa shirikisho la Kiprotestanti ulikubali kuandika katiba mpya ya kanisa "la kitaifa" Kanisa la Kijerumani la Kiinjili Deutsche Evangelische Kirche au DEK. Wakristo Wajerumani walimtaka kiongozi wao Ludwig Müller, aliyekuwa pia mshauri wa Hitler kwa maswala ya kidini, achaguliwe kuwa askofu mpya wa kanisa la kitaifa.

Hitler mwenyewe alimtaka pia Müller kuchaguliwa kuwa askofu wa kitaifa. Baada ya kushindwa kufikia shabaha yake alikasirika akaamuru uchaguzi mpya ya sinodi na mabaraza ya wazee kote Ujerumani. Usiku kabla ya uchaguzi, Hitler alihotubia Waprotestanti kupitia redio kupigia kura wagombea waliokuwa upande wake.

Wakristo Wajerumani walishinda asilimia 70 - 80 ya viti vyote katika mabaraza na sinodi, isipokuwa katika makanisa manne ya kieneo na jimbo la Westfalia kwenye kanisa la Prussia, ambapo Wakristo Wajerumani hawakupata uwingi.

Ushindi huu wa uchaguzi uliwawezesha Wakristo Wajerumani kupata wajumbe wa kutosha katika sinodi ya kitaifa iliyoendesha uchaguzi wa Müller kuwa askofu wa kitaifa Reichsbischof. Chini ya usimamizi wa Müller kanisa la Prussia lilipitisha sheria ya kutengua wachungaji na watumishi wote wenye ukoo wa Kiyahudi na hata watumishi waliowahi kuoa wake wasiotazamiwa kuwa Waarya mtu yeyote mwenye wazazi wa babu /bibi Myahudi hakuwa "Arya" bila kujali dini yake mwenyewe kufuatana na sheria za Wanazi.                                     

2. Kanisa la Ungamo

Sheria kuhusu Waarya kilisababisha hisia kati ya wachungaji. Chini ya uongozi wa Martin Niemöller, Ligi ya Dharura ya Wachungaji jer. Pfarrernotbund iliundwa, kwanza kwa kusudi la kusaidia wachungaji wenye asili ya Kiyahudi, lakini ligi hiyo ilibadilika kuwa mkusanyiko wa wapinzani dhidi ya kuingilia kwa Wanazi katika maswala ya kanisa. Uanachama wake uliongezeka wakati pingamizi na maneno ya Wakristo Wajerumani yaliongezeka. Msingi wa upinzani wa Ligi ya Dharura ya Wachungaji ulikuwa walichoona kama dharau ya ubatizo. Walitetea tofauti baina ya Wayahudi na Wakristo waliowahi kuwa Wayahudi wakiwaona kama wakristo kamili bila kasoro yoyote.

Mwanzoni Waprotestanti katika ligi ya dharura hawakupinga bado hatua zilizoichukuliwa na Wanazi dhidi ya Wayhudi kwa ujumla, zilizoanza kutungwa na kutekelezwa tu polepole. Hatimaye, Ligi ilibadilika na kuwa Kanisa la Ungamo.

Mnamo tarehe 13 Novemba 1933 mkutano wa Wakristo wa Ujerumani ulifanyika katika uwanja wa michezo huko Berlin, ambapo wasemaji walitangaza umoja wa Unazi na Ukristo, madai ya kuwafukuza wachungaji wote wasioshikamana na siasa ya Hitler, kufukuzwa kwa Wakristo wote wenye asili ya Kiyahudi katika kanisa, kuondolewa kwa Agano la kale katika Biblia ikiwa ni "kitabu cha Kiyahudi", na kubadilisha mahubri kuhusu Yesu anayepaswa kuonyeshwa kama shujaa aliyepinga athira mbaya ya Wayahudi.

Habari za mkutano huu zilishtusha wakristo wengi walioona hapa jaribio la serikali na chama cha utawala kuingilia maswali ya imani ndani ya kanisa.

Wakati Hitler, mwanasiasa kamili, alisita kutumia mabavu mno katika kipindi hiki cha mwanzo wa utawala wake, askofu Ludwig Müller aliwafukuza kazi na kuwahamisha wachungaji wanaoshikilia Ligi ya Dharura, na mnamo Aprili 1934 alitangaza kuondolewa kwa wakuu wa kanisa la Württemberg na wa Bavaria.

                                     

2.1. Kanisa la Ungamo Ungamo la Imani la Barmen

Mnamo Mei 1934, upinzani dhidi ya Wakristo Wajerumani ulikutana katika sinodi huko Barmen. Wajumbe walimshutumu Müller na uongozi wake na kutangaza kwamba wao na sharika zao ndio Kanisa la Kiinjili la kweli la Ujerumani. Ungamo la Barmen liliandikwa na Karl Barth, baada ya kushauriana wachungaji wengine kama Martin Niemöller na sharika kadhaa. Lilithibitisha kwamba kanisa si "chombo cha Serikali" na kwamba wazo la serikali kudhibiti kanisa lilikuwa mafundisho ya uwongo. Ungamo hilo lilisema kwamba serikali yoyote - hata ile ya kiimla - lazima ina kikomo wakati inakabiliwa na amri za Mungu. Tamko la Barmen lilikuwa msingi wa Kanisa la Ungamo.

Baada ya Ungamo la Barmen, kulikuwa na harakati mbili zilizopingana katika Kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani:

 • Kanisa la Ungamo Bekennende Kirche, BK
 • harakati ya Wakristo Wajerumani na

Kanisa la Ungano lenyewe halikulenga kuangusha serikali ya Wanazi, bali ilikaza upinzani dhidi ya majaribio ya serikali kuamulia mambo ya ndani ya kanisa na imani.

Lakini idadi ya wafuasi wake ilikuwa waliotambua kwamba misingi ya Unazi ilikuwa pamoja na upagani, na matendo mengi ya serikali ya Kinazi yalikuwa jinai mbele ya maadili ya Kikristo.                                     

2.2. Kanisa la Ungamo Baada ya Barmen

Hali hiyo iliendelea kuwa tata baada ya Barmen. Ukosefu wa uwezo upande wa Müller katika maswala ya kisiasa haukumpendeza Hitler. Mkutano wa Berlin ulileta aibu kwa chama cha Wanazi.

Hitler alijaribu kutuliza hali hiyo katika msimu wa 1934 kwa kuwaruhusu maaskofu wa Bavaria na Württemberg kuondoka tena katika nyumba zao walipowahi kubanwa. Alimchoka Müller na Wakristo Wajerumani akaondoa madaraka ya Müller haswa na Wakristo Wajerumani kwa jumla, akaunda Wizara mpya kwa ajili ya makanisa akamteu waziri mwenye uwezo mzuri zaidi wa kuongea na Wakristo.

Mwaka 1936 Kanisa la Ungamo, chini ya uongozi wa Niemöller, lilitoa barua kwa Hitler. Kwa lugha ya heshima ilipinga mielekeo ya serikali dhidi ya Ukristo, ililakamika kuhusu siasa ya kuwabagua Wayahudi na kudai serikali iache kuingilia katika mambo ya ndaniy a kanisa.

Serikali ilijibu kwa:

 • kumuua Dk. Friedrich Weißler, meneja wa ofisi na mshauri wa kisheria wa ofisi kuu ya Kanisa la Ungamo kambi ya wafungwa ya Sachsenhausen
 • kupiga marufuku matoleo kwa ajili ya Kanisa la Ungamo
 • kunyanganya fedha za Kanisa la Ungamo
 • kuwakamata wachungaji mia kadhaa

Waziri wa mambo ya kanisa aliwahotubia viongozi wa kanisa rasmi kwenye 13 Februari 1937 kwa maneno yafuatayo: Ukristo halisi ni sawa na "Ujamaa wa Kitaifa" na Ujamaa wa kitaifa ni kutenda mapenzi ya Mungu. Nimeambiwa kwamba Ukristo ni imani katika Kristo kama mwana wa Mungu. Hii inanifanya nicheke. Ukristo hautegemei Imani ya Mitume lakini inawakilishwa na chama cha NSDAP. Wajerumani sasa wanaitwa na Kiongozi =Hitler kufikia Ukristo wa kweli. Kiongozi ndiye kijumbe wa ufunuo mpya"

                                     

3. Matokeo

Baadhi ya viongozi wa Kanisa la Ungamo, kama vile Martin Niemöller au Heinrich Grüber, walipelekwa kwenye kambi za wafungwa. Wakati Grüber na Niemöller walinusurika, sio wote waliokoka: Dietrich Bonhoeffer alinyongwa kwenye Aprili 1945. Hii iliwaacha Wakristo ambao hawakukubaliana na Wanazi bila uongozi.

Wachache wa Kanisa la Ungamo walihatarisha maisha yao kusaidia Wayahudi kujificha kinyume cha sheria huko Berlin wakati wa vita. Walikusanya pesa na vitambulisho vilivyobadilishwa na waghushi na kupewa Wayahudi waliojificha ili waweze kupita kama raia halali wa Berlin. Washiriki kadhaa wa Kanisa la Ungamo walikamatwa na kuhukumiwa kwa sehemu yao katika kuunda vitambulisho vya kughushi, pamoja na Franz Kaufmann aliyepigwa risasi, na Helene Jacobs, ambaye alifungwa jela.

Baada ya Vita Kuu ya Pili, Azimio la Hatia la Stuttgart lilikuwa tangazo lililotolewa mnamo 19 Oktoba 1945 na Baraza la Kanisa la Kiinjili la Ujerumani Evangelische Kirche in Deutschland au EKD, ambapo ilikiri hatia ya kutokufaa kwake kwa kupingana na Wanazi na utawala wao. Iliandikwa haswa na washiriki wa zamani wa Kanisa la Ungamo.

                                     
 • ikieleza haja ya mabadiliko hayo. Ungamo hilo ni thibitisho tosha la nia ya Walutheri wa kwanza ya kubaki ndani ya Kanisa pekee linaloonekana. There is
 • watu. Katekisimu ya Kanisa Katoliki ina sehemu kuu nne: Ungamo la imani ufafanuzi wa Kanuni ya imani ya mitume Adhimisho la fumbo la Kikristo liturujia
 • yao. Hivyo katika Dola la Kijerumani yalikubalika rasmi maeneo yaliyoshikilia Ungamo la Augsburg na yale yaliyobaki katika Kanisa Katoliki, lakini si wenye
 • Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV 1265 - 1268 Ndipo Papa Gregori
 • Wajesuiti walikuwa washauri hasa wa watawala Wakatoliki. Waliposikiliza ungamo la dhambi zao walipata nafasi nzuri ya kuwapa mawazo na kusababisha hatua
 • Kanuni ya imani, au Ungamo la imani, au Tamko la imani, au Nasadiki Ukristo au Shahada Uislamu ni fomula iliyopangwa kwa muhtasari ili wafuasi wa dini
 • siku ili kuyaelewa, kuyatafakari, kuyaitikia na kuyashangilia. Mara nyingi inafuata hotuba, halafu ungamo la imani na maombezi kwa ajili ya watu wote.
 • Kikanisa. Ungamo la Augsburg ni mafundisho yaliyotungwa mwaka 1530 wafuasi wake walipodaiwa kujieleza mbele ya Bunge ili kurudisha umoja wa Kanisa Lengo
 • yao. Hivyo katika Dola la Kijerumani yalikubalika rasmi maeneo yaliyoshikilia Ungamo la Augsburg na yale yaliyobaki katika Kanisa Katoliki, lakini si wenye
 • yao. Hivyo katika Dola la Kijerumani yalikubalika rasmi maeneo yaliyoshikilia Ungamo la Augsburg na yale yaliyobaki katika Kanisa Katoliki, lakini si wenye
                                     
 • Apostolicum ni ungamo la imani ya Ukristo lililoanza kutumika mjini Roma katika karne ya 2 kwa ajili ya ubatizo, halafu likaenea hasa katika Kanisa la Magharibi
 • Patriarki wa Kanisa Katoliki la madhehebu ya Misri kati ya mitaguso mikuu miwili ya kwanza. Maisha yote ya Atanasi yalihusika na juhudi kubwa za Kanisa kwa ajili
 • niliyoiungama nilipozaliwa upya, Nishike ungamo lake nililolitamka nilipobatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Niweze kukuabudu wewe
 • ufashisti, na mwanzilishi mmojawapo wa Kanisa la Ungamo nchini Ujerumani. Maandishi yake juu ya jukumu la Ukristo katika ulimwengu wa kisasa yamekuwa
 • Utakase, ulinganishe taifa lako katika imani ya kweli na ungamo sahihi, na kuangaza mioyoni neno la mafundisho yako. Kwa kuwa ni zawadi yako kutuchagua tuihubiri
 • kufaulu kumuondosha Patriarki wa Kostantinopoli aliyetaka kuhalalisha ungamo la imani la Wakalvini. Idara ya Papa ilistawisha pia misheni za Waoservanti chini
 • Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Lk 1: 42 - 43 Ungamo hilo la Elizabeti likakamilishwa na Mtume Thoma aliyemuambia Yesu mfufuka: Bwana
 • Khristós, Kristo na λογία, logia, elimu ni tawi la fani ya teolojia linalochunguza hasa imani ya Kanisa kuhusu nafsi na hali za Yesu Kristo kwa kutegemea
 • interpretations.. Katika karne za kwanza za Kanisa imani hiyo inakiriwa na Kanuni ya Imani ya Mitume Italia na Ungamo la Imani la Atanasi Misri Ilifundishwa pia


                                     
 • utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni Math 16: 17 - 19 Ungamo la namna hiyo linaripotiwa na Yoh 6: 68 pia: Bwana Twende kwa nani? Wewe
 • na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli, uliothibitisha na kuongezea ungamo la Nisea katika Kanuni ya imani ya Nisea - Konstantinopoli. Mwaka 383, Kaisari

Users also searched:

kanisa la ungamo, kanuni. kanisa la ungamo,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →