Back

ⓘ Sethembile Msezane ni msanii, mshereheshaji na muongeaji wa Afrika ya Kusini anayetambulika zaidi kutokana na kazi za sanaa. Msezane anatumia ujuzi wake katika ..Sethembile Msezane
                                     

ⓘ Sethembile Msezane

Sethembile Msezane ni msanii, mshereheshaji na muongeaji wa Afrika ya Kusini anayetambulika zaidi kutokana na kazi za sanaa.

Msezane anatumia ujuzi wake katika fani mbalimbali inayojumuisha upigaji picha, filamu, uchongaji sanamu na uchoraji kuweka bayana masuala ya kidini, kisiasa na Ujuzi wa Kiafrika. Sehemu ya kazi zake zimelenga mchakato wa utengenezaje fikra na ushawishi katika utengenezaji wa historia Pamoja na ukosefu wa umbo halisi la mwanamke katika simulizi na nadharia ya uhalisia wa kumbukumbu za kihistoria. Kazi za Msezane zipo katika makumbusho ya Afrika kusini pamoja na dunia nzima na ameshinda tuzo nyingi. Msezane ni mwanachama wa ’iQhiya Collective’’, mtandao wa wanawake weusi ambao ni wasanii kutoka Cape Town, Johannesburg na kwingineko Afrika Kusini.

                                     

1. Elimu & Kazi

Japokuwa ni mzawa wa Kawazulu-Natal, Msezane alikulia Johannesburg. Baadaye alihamia Cape Town, ambako alijiunga na chuo kikuu cha ’Michaelis School of Fine Art’’ kusoma shahada ya sanaa mwaka 2012 kisa shahada ya uzamili mwaka 2017. Maonyesho ya Msezane yanalenga ukosekanaji wa wanawake katika siasa na mandhari ya historia nchini Afrika Kusini. Kupitia maonyesho yake, anaelezea ni kwa namna gani wanawake wamekua wakizuiwa na jamii katika jitihada zao, mavazi na kufanya utambuzi kwa kutumia mwili wake kama sanamu kwa kuvaa kama kiashiria kwenye mavazi kukazia umuhimu wwake, uwepo na uhusika katika sehemu za wazi.

Kazi za Msezane zimetambulika kwa kiasi kikubwa ulimwenguni kwote na katika makumbusho ya Afrika Kusini ikiwemo ’Iziko South African National Gallery’’, ’Zeitz Museum of Contemporary Art Africa’’ na ’University of South Africa’’. Mwaka 2016 Msezane alikua mtu wa kwanza kupata tuzo ya ’Rising Light Award’’ wakati wa tuzo za Mboko. Alipata pia tuzo za TAF na SYLT Emerging Artist Residency TASA mwaka huohuo na alifika kumi bora mashindano ya Barclays Latelier. Msezane aliteuliwa pia katika tuzo za ’ANTI – Contemporary Art Festival’’ mwaka 2017.

Kazi yake, "Chapungu-the Day Rhodes Fell" 2015 ilionyeshwa wakati wa maandamano ya ’Rhodes Must’’, wakati huo sanamu ya John Cecil Rhode iliyopo Chuo kikuu cha Cape Town ilikua ikiodolewa. Msezane alisimama kama sanamu mtu kwa muda wa masaa katika maonyesho ya kutaka kuchukua nafasi ya sanamu ya Rhodes. Msezane amekua akitumia siku za mapumziko nchini Afrika Kusini kutumbuiza na kuelezea juu ya masuala yanayo athiri vijana wa sasa, hii ilikua ni kama sehemu ya maonyesho yake ya "Public Holiday 2014-2015" Maonyesho mengine ya Msezane inajumuisha "Kwasuka Zukela" 2017 Maonyesho ya MoMo, Cape Town, Afrika Kusini, "All Thing being Equal" Zeitz Mocca 2017Cape Town, Afrika Kusini na "Unframed"2018 katika maonyesho ya sanaa ya Cape Town. Msezane alifanya maonyesho yake ya kwanza nchini Uingereza "Speaking through the wall" katika makumbusho ya Tyburn Gallery, London 2019, pamoja na kazi yake mpya ya "Signal her return III" huko Nottingham, Uingereza.

Msezane pia amefanya maonyesho ya vikundi baadhi zikiwa kama "Womens Work and the art of Disruptions"2016 huko Iziko Afrika Kusini, "Re-assisting narratives’’2016 Amsterdam, "Dancing on a Volcano"2018 Nigeria, "Translations" 2015 Portland, Oregon, "Made Visible: Contemporary South African Fashion and Identity" 2019, Boston, Marekani.

Msezane alikua kama muongeaji kwenye TedGobal mwaka 2017.

                                     

2. Maonyesho

"Speaking Through the Wall" 2019 Tyburn. London, Uingereza

"Kwasuka Sukela" 2017 Momo. Cape Town, Afrika Kusini

"All Things Being Equal" 2017 Zeitz Mocca. Cape Town, Afrika Kusini

"Unframed" 2018 Cape Town Art Fair. Cape Town, Afrika Kusini.

"Umoya: a Quiet revolution" maonyesho ya sanaa ya FNB Joburg. Johannesburg, Afrika Kusini

"Reassisting Narratives" 2016 Framer Framed, Amsterdam, Uholanzi

Users also searched:

sethembile msezane, jamii. sethembile msezane,

...

Encyclopedic dictionary

Translation
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →